
Wizara ya Sheria na Katiba nchini, imeendesha warsha kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu kanuni za ulinzi wa watoa taarifa na mashahidi.
Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo tarehe 24 Juni 2023, mkoani Singida.
Wizara hiyo imelenga zaidi katika kufafanua kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Mtoa taarifa na Mashahidi, kuimarisha uelewa wa wahariri na umuhimu wao, masharti na athari kwenye uandishi wa habari za uchunguzi.
Pia wizara hiyo imeeleza maarifa na zana muhimu za kuwalinda watoa taarifa na mashahidi ipasavyo, kuwawezesha kuripoti masuala nyeti bila kuathiri usalama wa vyanzo vyao.
Be the first to comment