Wanachama TEF wakutana kujadili kazi za taasisi yao

WANACHAMA wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wamekutana kujadilia na kupitia kazi mbalimbali za jukwaa hilo.

Mkutano huo umefanyika jijini Dare es Salaam tarehe 15 Oktoba 2022 katika Ukumbi wa Hoteli ya Peacock, ambapo zaidi ya wajumbe 70 walishirki.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na miradi, mapitio ya matumizi ya fedha na mipango ya baadaye.

Mkutano huo uliongozwa na Deodatus Balile, mwenyekiti wa jukwaa hilo pia baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya TEF.

Pamoja na kazi zingine, Balile aliwaptisha wajumbe hao kwenye miradi mbalimbali iliyofanywa na jukwaa hilo pia kutoa maelezo kuhusu miradi iliyopita, iliyopo na ijayo.

Kwenye mkutano huo, wajumbe walitapa fursa ya kuchangia mawazo kuhusu miradi ambayo ilifanywa na TEF na ile iliyopo.

Lilian Timbuka, Mjumbe wa Bodi ya TEF pia Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi alieleza kuwa, mradi unaohusu  sheria ya ndoa unapaswa kufanywa kwa juhudi kubwa ili kuokoa watoto wanaolawitiwa, kubakwa na wale wanaoingia kwenye ndoa za utotoni.

‘‘Wahariri kuna mambo amabayo hata shetani amejiwekea mipaka, mambo ya watoto kulawitiwa, kubakwa na hata ndoa za utotoni tunapaswa kuwa nayo ‘serious,’’ alisema.

Salim Said Salim, Mhariri Mkongwe na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF alisema, wahariri wanapaswa kujua sheria kwa undani kuhusu miradi inayohusu jamii ikiwemo sheria zinazohusu haki za watoto.

Daniel Mbega kutoka Gazeti la Tanzania Leo alishauri , ni vizuri kujiridhisha na habari zinazohusu watoto hasa katika ubakaji akifafanua kuwa, taarifa zingine hutawaliwa na fitna na migogoro ya familia hivyo usingiziwaji unahusika.

Mjumbe mwingine Godfrey Lutego alishauri, waandishi wanaoripoti habari za matukio ya kusikitisha ya watoto, wabebe hisia ya kile wanachoripoti.

 

 

 

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*