Waandishi wapewa mafunzo uandishi habari za UVIKO-19

Wanahabari kutoka mikoa mbalimbali nchini, wamepata mafunzo ya namna ya kuandika habari zinazohusu maambukizi ya Virusi vya Korona (UVIKO-19), jijini Dodoma.

Mafunzi hayo ya siku mbili, yameendeshwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) leo tarehe 18 Agosti 2022.

Juliana Mshama, mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya katika Kitengo cha Elimu kwa Umma amesema, wanahabari nchini wanapaswa kuendelea kuhamasisha wananchi kujikinga na virusi hivyo sambamba na kupata chanjo.

“Takwimu zinaoneshe kwamba, bado kuna maambukizi ya UVIKO-19, jamii inapaswa kuendelea kuelimishwa namna ya kujikinga ikiwa ni pamoja na kupata chanjo.

“Mtu akiwa amepata chanjo anakuwa katika mazingira mazuri ya kutoumizwa na virusi hiyo. Ni muhimu kupata chanjo ili kubaki salama,” amesema Mshama.

Amesema, idadi ya watu waliopata chanjo ya UVIKO– 9 nchini imefika zaidi ya nusu ya watu wenye umri kisheria (kuanzia miaka 18 na kuendelea) wa kupata chanjo na kwamba, wanawake wanaongoza kujitokeza kuliko wanaume.

“Mpaka sasa asilimia 51.92 ya Watanzania wamepata chanjo ya UVIKO-19. Wanawake waliopata chanjo ni asilimia 54 huku wanaume wakiwa asilimia 46.

“Kwenye orodha ya mikoa, mkoa wa kwanza kwa watu wake kuhamasika kupata chanjo ni Dodoma ambapo wana asilimia 85 ya waliochanja, lakini mkoa unaoshika mkia kwa watu wake kujitokeza ni Songwe ambapo ni asilimia 18.6 tu waliojitokeza,” amesema Mshuma.

 

Pia amesema, hadi kufikia Disemba mwaka huu, serikali inatarajia kuchanja watu milioni 21 sawa na asilimia 70 ya Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi.

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amewataka wanahabari kuandika habari za UVIKO-19 kwa undani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*