UTT: Kuna fursa kubwa ya uwekezaji huku kwetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Uwekezaji nchini UTT AMIS, Simon Migangala ametoa wito kwa Watanzania kuwekeza mitaji yao kwenye taasisi hiyo kwa kuwa, kuna manufaa makubwa na ya haraka kulingana na malengo.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Julai 2023, jijini Dar es Salaam wakati taasisi hiyo ilipokutana na wahariri kwa ajili ya kuelezea mikakati yao na faida ya taasisi hiyo kwa Watanzania.

“UTT kuna faida kubwa katika uwekezaji, kwa urahisi zaidi nenda Benki ya CRDB, NMB, NBC ama Exim ueleze unataka kuwekaza kupitia UTT. Kwenye taasisi hii unaweza kupata faida kila mwezi, mwaka ama kwa kadiri utakavyotaka, ni rahisi sana.

“Kuna uwekezaji wa aina mbalimbali, Ukifika UTT ama benki unaweza kueleza malengo yako ya muda mrefu halafu utafafanuliwa kwamba, ili uweze kufikia malengo hayo unapaswa uwekeze kwa namna gani na wengi wamefanikiwa,” amesema.

Katika uwekezaji UTT, mwekezaji Anaweza kuona pesa yake inaongezeka kila simu na kwamba, ni rahisi kuwekeza kulingana na malengo yao.

“Unaweza kuwa unachukua faida kila mwezi, inategemea na malengo yako. Ukiwekeza UTT AMIS, faida yake unaweza kuiona moja kwa moja kwenye simu yako,” amesema na kuongeza:

“Tunaweza kukadiria kwamba kwa sasa tuna wawekezaji zaidi ya 300,000 na kila siku watu wanaongezeka ndiyo sababu hata ofisini kwetu, kumekuwa na ongezeko la watu wanaofika kujisajili.”

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*