
Naysan Sahba, Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya kulinda haki za watoto.
Sahba ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Mei 2023 alipokutana na baadhi ya wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kufanya mazungumzo kuhusu majukumu yanayofanywa na shirika hilo pia miradi ya UNICEF na TEF.
“Amani iliyopo Tanzania imeweka mazingira mazuri ya utekelezaji na ulinzi wa haki za watoto, ni tofauti na nchi kama Syria, Yemen, Sudan na kwingine.
“Naona mazingira mazuri katika ulinzi wa haki za watoto katika utawala wa Rais Samia (Suluhu Hassan),” amesema.
Be the first to comment