
GERSON Msigwa, Msemaji wa Serikali amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari nchini, umefika hatua nzuri.
Msigwa alitoa kauli hiyo tarehe 19 Septemba 2022, alipoulizwa na mwandishi kuhusu hatua inayofikiwa baada ya kikao cha wadau kilichofanyika tarehe 11 na 12 Agosti 2022.
“Mchakato umefika hatua nzuri, tutatoa taarifa nini kinaendelea,” alisema Msigwa huku akisisitiza “mtajulishwa.”
Hata hivyo, kikao cha wadau kilichofanyika tarehe 11 na 12 Agosti 2022, kiliafikiana baadhi ya vipengele vya sheria ya habari, huku vingine wakishindwa kufikia muafaka.
Tarehe 26 Agosti 2022, Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari alisema, serikali itapeleka mapendekezo hayo bungeni baada ya kukubaliana na wadau wa habari nchini.
Be the first to comment