TEF yawakutanisha wanahabari na washauri wao

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), leo limeendesha semina ya siku moja kwa waandishi wa habari na washauri wa waandishi hao kwa lengo la kuongeza ubora wa habari zinazohusu Kampeni ya Utetezi wa Sheria ya Vyombo vya Habari nchini.

Semina hiyo iliyoendeshwa na Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF na Neville Meena, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, imefanyika jijini Dar es Salaam.

Katika semina hiyo, wanahabari wameelezwa umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya karibu na washauri wao ili kuinua ubora wa taarifa wanazozichapa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.

‘‘Mshauri anajitolea sehemu ya wakati wake ili kukusaidia na kukujienga kwa manufaa ya sasa na hata hapo baadaye, ni vizuri kuwa na amwasiliano ya karibu na mshauri wako,’’ amesema Meena na kuongeza;

‘‘Tunapaswa kuwa na stori ambazo hata hapo baadaye, wengine watakaokuja watajua kuna kazi iliyofanywa. Kwa kiwango kikubwa katika ushirikiano huu, mwanahabari anaweza kufaidika kwa kiwango kikubwa endapo atafanya kazi kwa karibu na mshauri wake,’’ amesema.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa Balile amesema, anaamini muswada wa sheria ya habari utafikishwa bungeni Novemba mwaka huu.

‘‘Hatutaki kuamini kwamba, muswada utapelekwa bungeni Februari mwakani, tunaamini kuwa muswada huo utapelekwa bungeni katika Bunge la Novemba mwaka huu,’’ amesema Balile.

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*