
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) leo tarehe 25 Agosti 2022, limefanya kikao chake cha pili kwa ajili ya kuweka mikakati ya ndani na nje ya jukwaa hilo.
Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za jukwaa hilo, Mtendeni jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa na wajumbe wa jukwaa waliochaguliwa kwa ajili ya kuunganisha mawazo mkakati ili kufikia malengo.
Kikao hicho kimeongozwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo Deodatus Balile. Wajumbe wengine waliohudhuria ni Yasin Sadiq (Hoja), Dk. Darius Mukiza (Mkufunzi UDSM), William Shao (Mwananchi), Angela Akilimali (Uhuru).
Wengine ni Joseph Kulangwa (Raia Mwema), Yusuph Katimba (TEF), Neville Meena (Farmer) na Anita Mendoza (Kaimu Mtendaji Mkuu TEF).
Be the first to comment