TEF yasikitishwa uvamizi meza za magazeti

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limelaani vitendo vya askari wa Jiji la Dar es Salaam kunyanyasa na kupora meza za wauza magazeti.

Taarifa ya jukwaa hilo leo tarehe 22 Juni 2022  imeeleza, wanamgambo hao walivamia meza za wauza magazeti jijini humo tarehe 21 Juni 2022, bila kutoarifa ama sababu.

“Ikumbukwe kwamba Oktoba mwaka jana, serikali ilianza kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) pembezoni mwa barabara za Jiji la Dar es Salaam, lakini wauza magazeti hawakuondolewa si kwa bahati, bali kwa mujibu wa Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Mwaka 2014 nyongeza ya 9(3) HSC 4902.90.00 inayotambua magazeti kuwa ni nyenzo ya elimu si biashara,” imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deodatus Balile.

Mwenyekiti huyo ameeleza, unyanyasaji wa namna hiyo haukubaliki.

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*