
WAJUMBE tisa wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wamekutana kujadili na kuweka mpango mkakati wa miaka minne wa taasisi hiyo.
Mpango mkakati huo umelenga kuinua tasnia ya habari, wanahabari pamoja na kuweka mazingira ya kuwezesha taasisi hiyo kujiendesha.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 13 Agosti 2022, katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Kisutu, jijini Dar e Salaam.
Waliohudhuria kikao hicho ni Stella Aron (Jamhuri), William Shao (Mwananchi), Joseph Kulangwa (Raia Mwema), Neville Meena (Farmer Magazine), Yassin Sadiq (Hoja), Yusuph Katimba (TEF Digital), Anita Mendoza (Kaimu Mtendaji Mkuu TEF) na Dk. Darius Mukiza (Chuo Kikuu).
Kwenye kikao hicho, wamejadili mapendekezo mbalimbali na kukubaliana namna ya kuyaendea.
Be the first to comment