TEF, UN wakubaliana mambo matano

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Mataifa (UN), wamekubaliana utekelezwaji wa mambo matano katika safari ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (MDGs) 2030.

Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mkutanio wa UN na Wahariri uliofanyika tarehe 10 Februari 2023. TEF iliwakilishwa na mwenyekiti wake Deodatus Balile huku UN ikiwakilishwa na Zlatan Milisic, ambaye ni mwakilishi wa umoja huo nchini Tanzania.

Zlatan Milisic, Mwakilishi wa UN, Tanzania

Mambo waliyokubaliani TEF na UN ni pamoja na kuanzisha Kikosi Kazi cha pamoja ili kuunda ushirikiano wa kujengea uwezo vyombo vya habari katika utoaji taarifa zinazohusu maendeleo (UNSDCF).

Kuendesha mafunzo kwa wahariri na waandishi katika kuandika habari zinazohusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ndani ya nchi.

Jabir Idrisa, Mhariri MwanaHalisi akichangia mada

Pia wamekubaliana kuendesha mafunzo kuhusu namba bora ya kuripoti chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Jambo la nne walilokubaliana ni UN kuandika taarifa zake kwa Lugha ya Kiswahili, pia kushirikisha vyombo vya habari ili taarifa hizo ziweze kuchapishwa kwa wakati.

Joyce Shebe, Mhariri Clouds akizungumza kwenye mkutano huo

Mwisho ni wahariri kuwa sehemu ya taarifa za Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG media compact) ili kuingiliana kwa karibu na UN na kuweza kupata taarifa kwa namna zinavyohitajika kwa mhariri mwenyewe.

Kwenye mkutano huo, Balile amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kuhakikisha, vinafuatilia ahadi zinazotolea na taasisi za kimataifa.

Deodatus Balile, Mwenyekiti TEF akizungumza kwenye mkutano huo

“Tunalenga kuinua heshima ya vyombo vya habari Tanzania, UN tumekutana nao hapo kuhusu mpango wao wa 2023 – 2027 ndani ya nchi yetu ili kujua hatua kwa hatua katika utekelezaji wa mipango yao.

“Tunapaswa kuyajua maeneo ya mkakati na namna wanavyotekeleza. Sisi kama vyombo vya habari jukumu letu ni kuhakikisha tunafuatilia je, wanatekeleza kama walivyoahidi?,” amesema Balile.

Dk. Darius Mukiza akisoma mapendekezo ya TEF

Akizungumzia kwenye mkutano huo, mwakilishi wa UN, Zlatan amesema, vyombo vya habari vinapaswa kuwa karibu na jamii ili kushiriki katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto, wanawake lakini pia mila potofu.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*