Serikali yapongezwa kuwasilisha Muswada Sheria ya Huduma za Habari

MWENYEKITI  wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameishukuru serikali kwa kuwasilisha Muswada wa Mapendekezo ya Sheria ya Huduma za Habari bungeni leo tarehe 10 Februari 2023.

Akizungumza na Wanahabari katika ofisi za jukwaa hilo jijini Dar es Salaam, Balile amesema pamoja na kuwasilishwa kwa muswada huo, wakikabidhiwa makala yake wataupitia kuona kama yake yaliyopendekezwa na wadau wa habari yamezingatiwa.

“Mpaka sasa hatujapata makala ya muswada huo. Tukiipata tutawaiteni tena kuwaeleza kama yake yaliyopendekezwa yamo ama la,” amesema Balile.

Amesisitiza kuwa, TEF inapigania uhuru wa habari si kwa faida ya wanahabari pekee, bali ni uhuru wa kila mtu kujieleza.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*