Muswada wa Habari kusomwa tena Aprili – Nape

NAPE Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema, anatarajia bunge lijalo (Bunge la Aprili) litasoma Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Hudumna za Habari kwa mara ya pili.

Amesema, watu wengi walitarajia kwamba, muswada huyo ungewasilishwa peke yake, lakini haikuwa hivyo na kwamba, uliwasilishwa ndani ya muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali.

“Sheria ilisomwa bungeni na tunategemea itasomwa tena kwenye Bunge lijalo kwa mara ya pili. Ikisomwa kwa mara ya kwanza inakuwa ni public document (nyaraka ya umma), wanapewa kamati ya Bunge na wadau wanapata fursa ya kuujadili.

“Tunategemea kwenye Bunge lijalo utajadiliwa na muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza baada ya majadiliano na wanahabari,” alisema Nape wakati akizungumza kwenye mjadala wa Mwananchi Twitter Space unaoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*