
DEODATUS Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema anatarajia Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Habari utasomwa bungeni Januari mwaka 2023.
Akizungumzia hatua mbalimbali ziliopitiwa na zijazo leo tarehe 4 Januari 2022, Balile amesema yalianza malalamiko ya wadau wa habari kuhusu sheria hiyo ya mwaka 2016 kuminywa uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Na kwamba, ingawa walianza tangu mwaka 2016 baada ya kuundwa sheria hiyo, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ndio imesikia kilio cha wadau wa habari na kuagiza mchakato uanze kufanyika ili kuondoa vipengele vya sheria hiyo.
Hata hivyo amesema, baada ya vikao vya wadau wa habari na serikali, kinachofuata ni uandishi wa muswada huo ambao hupita ngazi mbalimbali kabla ya kufikishwa bungeni.
“Kwanza kabisa utapitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kisha utajadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu na baada ya hapo utajadiliwa na Kamati ya Baraza la Mawaziri.
“Ukitoka hapo utajadiliwa na Baraza la Mawaziri, tunarajia itakuwa kati ya Januari 13 na 14, matazamio yetu ni kwamba utasomwa bungeni kwa mara ya kwanza Januari 31, mwaka huu kisha tutakutana na wadau kuzungumza na wabunge baadaye utasomwa kwa mara ya pili na utajadiliwa,” amesema Balile.
Amesema, hatua hiyo imefikiwa baada ya awali kukamilika kwa mafanikio makubwa.
Na kwamba, isingekuwa rahisi kuwa na matumaini hayo iwapo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ingeamua kuyapa mgongo malalamikiwa ya wadau wa habari nchini kuhusu vipengele vinavyozuia ukuaji wa sekta ya habari nchini.
Be the first to comment