MISA TAN yapongeza serikali kuelekea uhuru wa habari

MWENYEKITI wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), Salome Kitomari amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua kuelekea uhuru wa wanahabari kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.


Ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Mei 2023, jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya taasisi hiyo.

Amesema, mpaka sasa miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili tasnia ya habari nchini, ni pamoja na uchumi hafifu wa wanahabari.

“Waandishi wengi wana hali ngumu ya maisha, hawana mikataba, bima za afya, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Hali hii inaathari kubwa kwenye mchakato wa habari kwa kuwa, kunatoa mwanya wa rushwa. Siku zote, tumbo lenye njaa haliwezeshi ubongo kufikiri vyema,” amesema.


Kwenye maadhimisho hayo, Msemaji Serikali, Gerson Msigwa amesema, serikali inaendelea kuboresha mazingira ya vyombo vya habari.

Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Elizabeth Riziki amesema, taasisi hiyo ina matawi tisa ikiwa ni katika nchi za Zambia, Msumbiji, Malawi, Lesotho, Botswana, Namibia, Angola, Tanzania na Zimbabwe ambako ndiyo Makao Makuu ya matawi yote.

“MISA Tanzania kwa pamoja na wadau wa habari tunaangalia namna gani tunaweza boresha mazingira ya uhuru wa kujieleza kwa jamii nzima.

“Namna gani tunaweza kumleta mwandishi wa habari kwa jamii ili kuhakikisha kila mwana jamii anatumia haki yake vema,” amesema.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*