‘Media zijielekeze kwenye mijadala yenye tija’

VYOMBO vya habari nchini vimeshauria kujenga tabia ya kuanzisha mijadala yenye kuchochea ukuaji wa wa uchumu na sio mijadala isiyo na tija kwa nchi na wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na leo tarehe 22 jijini Dar es Salaam na Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakati akizungumzia umuhimu wa wanahabari kuchochea maendeleo, uzalishaji mali na mabadiliko ya sheria.

Balile alisema taarifa za ujenzi, uboreshaji wa viwanda, miundombinu na kilimo ambazo zitabadilisha maisha ya Watanzania kutoka katika umasikini zinapaswa kupewa nafasi zaidi kuliko zile za maisha binafsi ya watu na malumbano.

“Nchi zinazoendelea wanajadili namna ya kuuza biashara na viwanda vyao kwa kuzalisha bidhaa bora pamoja na kutafuta masoko, sisi hapa tuna viwanda, uzalishaji wa gesi lakini huoni mijadala mingi kwenye eneo hilo, tubadilike” alisema

Naye Walace Maugo, aliwataka waandishi wa habari wapiganie haki za Watanzania na kuboreha maisha yao kupitia taaluma yao na kazi wanazozifanya kila siku.

“Sisi ndiyo tunaotengeneza mijadala kwenye jamii, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha maisha bora yanapatikana na watu wanafurahia maisha katika nchi yao, tusijione wanyonge kuna hatua kubwa zimechukuliwa kutokana na kazi tunazozifanya” alisema

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*