‘Mapendekeo yakifanikiwa, yataleta athari kubwa’

IWAPO Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Habari yatafanikiwa, hata kama sio yote, yataleta athari kubwa kwenye sheria zingine za habari kwa kuwa, sheria hii (Huduma za Habari) ndio injini ya sheria nyingine.

Ni kauli ya Neville Meena, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), leo tarehe 27 Agosti 2022 wakati akizungumza na Radio Abood (Abood FM), Morogoro.

“Sheria iliyopo haikukubalika toka mwanzo. Kama mabadiliko ya sheria ya huduma za habari yatafanikiwa hata kama sio vipengele vyote kwa pamoja, ilaleta athari kubwa katika sheria zingine,” amesema Meena.

Kauli hiyo ilitanguliwa na maelezo kwamba, kwa sasa harakati za mabadiliko zimejikita katika Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka kwa kuwa, serikali imeeleza kuanza na sheria hiyo.

Amesema, ni jambo la kupongeza kwa hatua ambayo serikali imechukua na ilipofika mpaka sasa, kwani yapo ambayo wamekubakiana na yapo ambayo hawajakubaliana.

“Kama alivyosema mheshimiwa waziri (Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) wakati alipozungumza na BBC.

“Alisema yapo ambayo wameishakubaliana na mazungumzo bado yanaendelea. Sisi tunaamini kuwa, kuna athari chanya itatokea kwenye uandishi wa habari,” amesema.

Amesema, wadau wa habari wameanzisha mchakato huo kwa kuwa, wana nia nzuri na tasnia ya habari na kwamba, serikali imeona nia hiyo ndio maana imeingia kwenye mazungumzo.

“Sisi tuna nia nzuri na mjadala huu na ninaamini tutafika pazuri na kuifanya tasnia ya habari kuwa salama kwa wamiliki wa vymbo vya habari na wanahabari wenyewe.

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*