
Theophil Makunga (kulia), Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria kandamizi za habari nchini, unalenga kuweka mazingira mazuri kwa wanahabari na vyombo wanavyofanyia kazi.
“Mchakato wa mabadiliko haya, unalenga kuweka mipaka lakini pia uhuru wa habari bila kuumiza mtu yeyote. Tunalenga kupata uhuru zaidi wa habari na wajibu kwa mwanahabari.
“Tunapozungumzia uhuru wa vyombo vya habari, sio kwamba tunataka upendeleo kutoka serikalini, la! Tunacholenga hapo kila mmoja apate haki na awajibike,” amesema Makunga.
Amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu wa kupitia sheria za habari na kuagiza zifanyiwe maboreshio ili kuendana na mazingira yaliyopo, hivyo ni wakati wa kushikamana ili kufikia lengo la uhuru wa habari.
Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) pia mwenyekiti mstaafu wa jukwaa hilo, Theophil Makunga (kulia), akimkabidhi flashi yenye mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za habari Mhariri wa Gazeti la Majira, Ruben Kagaruki.
Theophil Makunga (kulia), Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na mwenyekiti mstaafu wa jukwaa hilo akimkabidhi flashi yenye mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za habari Mhariri wa Gazeti la Jamhuri, Joe Beda.
Wafanyakazi wa Gazeti la Jamhuri wakimsikiliza Makunga ambaye haonekani vizuri, alipokwenda ofisini kwao kuelezea malengo na hatua zilizofikiwa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria za vyombo vya habari nchini.
Mwenyekiti Mstaafu Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga (kushoto) akizungumza na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Tanzania Leo, Eckland Mwaffisi. Makunga alitembelea ofisi za gazeti hilo, jijini Dar es Salaam kueleza malengo na hatua ya mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari nchini ulipofika na unapoelekea.
Be the first to comment