Mabadilio ya Sheria za Habari; TEF yateua ‘kikosi kazi’ kuongoza waandishi

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limefanya kikao na wanataaluma washauri (mentors) wa habari kwa ajili ya kusimamia waandishi wa habari zinazohusu mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, kimefanyika leo tarehe 15 Julai 2022 katika Ofisi ya TEF, jijini Dar es Salaam.

Wanataaluma walioteuliwa kusimamia waandishi  ni  Joseph Kulangwa, Mhariri wa Raia Mwema; Stella Aron, Mhariri wa Majira; Rashidi Kejo, Mhariri wa Mwananchi; Angela Mang’enya, Mhariri wa TBC; Joe Nakajumo na Midladjy Maez; Wahariri Wastaafu.

Wanataaluma walioteuliwa kusimamia waandishi hao ni  Joseph Kulangwa, Mhariri wa Raia Mwema; Stella Aron, Mhariri wa Majira; Rashidi Kejo, Mhariri wa Mwananchi; Angela Mang’enya, Mhariri wa TBC na Joseph Nakajumo na Midladjy Maez ambao ni Wahariri Wastaafu.

Angela Mang’enya amepangwa kuwakufunzi Fatma Hassan Ali (Channel Ten), Kissa Daniel (East Africa Tv), Faridy Mohammed (Mlimani Tv), Godfrey Monyo (ITV).

Joseph Nakajumo atawasimamia Christopher James (Radio One), Salma Juma (Classic Fm), Philip Nyiti (Clouds Media) na Brumo Bomola (Radio Tumaini).

Rashid Kejo atakuwa na waandishi Regina Mkonde (Mwanahalisi Online), Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Brighter Davidi (Daily News Digital) na Iddy Lugendo wa Majira.

Joseph Kulangwa amepangiwa Alex Kazenga (Jamhuri Media), Peter Elias (Mwananchi), Mery Geofrey (Nipashe) na Goodluck Hongo wa Tanzania Daima.

Srella Aron atasimamia Anneth Nyoni (Tumaini TV), Humphrey Msechu (Spatklight TV), Jackline Martin (Times Majira) na Yusuph Digossi (IBN TV).

Kwenye timu hiyo, Maez atakuwa na kazi ya kupitia kazi na kuandika ripoti.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*