UVIKO-19 bado ipo, tuchukue tahadhari – Wizara Afya

WATANZANIA wametakiwa kubadili mienendo yao kwa kuwa, maambukizi ya Virusi Vya Korona (UVIKI-19) bado yapo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Juliana Mshama katika siku ya pili ya mafunzo ya uandishi wa habari za UVIKO-19, yaliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), jijini Dodoma leo tarehe 19 Agosti 2022.

Amesema, takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha kuendelea kuwepo kwa virusi hiyo huku akiomba jamii kuchukua tahadhari zaidi.

“Kwa siku sita (kuanzia tarehe 6-12 Agosti 2022) visa vipya vya maambukizi ya UVIKO-19 ni 123. Tuzidi kuchukua tahadhari kwa kufuata kanuni zilizoelekezwa,’’ amesema Mshama.

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*