Kongamano la TEF kupitia Muswada Sheria ya Habari

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limepanga kujalidi Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari kwenye kongamano lake litaloanza tarehe 29 – 31 Machi 2023, mjini Morogoro.

Muswada huo uliwasilishwa bungeni tarehe 10 Februari 2023, ambapo baadhi ya wadau wameeleza kutoridhishwa nao kwa kuwa, zaidi ya nusu ya vipengele walivyokubaliana kati ya serikali na wadau, havimo.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kongamanbo hilo, Neville Meena ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF amesema, kongamano hilo la siku nne, mgeni rasmi ni Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

“Miongoni mwa mada sita zitakazojadiliwa kwenye kongamano hili, ni pamoja na Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria za Habari na mweleko wake,” amesema Meena.

Mada zingine ni Utendaji wa Vyombo vya Habari, Taaluma na Maadili; Wanawake katika habari na hatari ya kutoweka kwako kwenye vyumba vya habari; Uchumi wa Vyombo vya Habari na jinsi ya kuvinusuru.

Pia Mabadiliko ya Teknolojia, Ukuaji na Ujenzi wa Mitandao ya Kijamii yenye viwango vya kitaaluma na Vyombo vya Habari na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Meena amesema, kongamano hili pia linatarajiwa kuhudhuriwa na Dk. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria.

Jane Mihanji, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF amesema, miongoni mwa sababu kuweka mada inayohusu wanawake na vyombo vya habari ni kutokana na tafiti kuonesha kwamba, kuna unyanyasaji wa wanawake kwenye vyombo vya habari.

“Tumekuwa tukihimiza kuwa na ushiriki sawa. Baadhi ya tafiti zinaonesha wanawake wanaopewa nafasi za juu ni wachache. Tafiti za TAMWA, Internews na zingine zinaonesha kuwa, kumekuwa na unyanyasaji wa wanawake kwenye vyumba vya habari.

“Taarifa zao zimekuwa hazitoki hivyo, wamekuwa wakikimbia vyumba vya habari,” amesema Jane.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*