Kilikua kilio cha muda mrefu – Nape

Marekebisho ya sheria ya Huduma ya Habari yaliyopitishwa leo tarehe 13 Juji 2023 na Bunge, yamekuja baada ya kilio cha muda mrefu tangu sheria hiyo ilipotungwa mwaka 2016.

Kwa wakati wote, wadau wa habari  wamekuwa wakilia ni lini sheria hiyo ingefanyiwa marekebisho.

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye ana dhamana na taaluma ya habari na vyombo vya habari, amesema wadau walipelekea mapendekezo katika vifungu 21, hata hivyo ni vifungu tisa ndivyo vilionekana kuhitaji marekebisho ya haraka.

“Wadau walileta mapendekezo 21, lakini wakati tunapitia tuliona marekebisho nane hayakuwa na ulazima hivyo tukayaacha kama yalivyo kwenye sheria ya awali lakini mengine tisa yalifanya marekebisho ikiwemo kuondoa jinai katika makosa ya kashfa (defamation),” amesema Nape.

Waziri Nape amesema sheria imetoa nafasi kwa waandishi kuweka taaluma yao kama chombo kinachotambulika pamoja na kuwepo waandishi wenye sifa ili watoe habari zenye kuwatosheleza walaji.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*