Jaji Feleshi: Lengo taaluma ya habari kuwa kama zingine

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Eliezer Feleshi amesema, licha ya kelele nyingi katika sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, lakini lengo kuu ni kuifanya taaluma hiyo kuwa kama zilivyo vyingine.

Mwanasheria Mkuu ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumanne Juni 13, 2023 wakati akijibu hoja za wabunge katika muswada wa sheria ya huduma za habari aliouwasilisha bungeni kwa lengo la kufanya marekebisho katika vifungu 9.

Hata hiyo Dk Feleshi amesema muswada huo umeondoa mambo mengi ambayo yalikuwa na kero kwenye sheria hiyo ikiwemo adhabu kubwa za vifungo na faini walizokuwa wakikabiliana nazo waandishi.

Amewaambia wabunge kuwa, sheria inayorekebishwa licha ya kuwepo kwa ukomo wa baadhi ya mambo, lakini imetazama kwa kiasi kikubwa kada hiyo ili kuwafanya waandishi wawe huru katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Miongoni mwa adhabu zilizopunguzwa ni pamoja na eneo lililotaja kifungo cha kati ya miaka 5 hadi 10 ambapo sasa itakuwa miaka 2 hadi 5 wakati faini inashuka hadi Sh3 milioni na ukomo ni Sh10 milioni katika adhabu iliyokuwa ikienda hadi Sh20 milioni.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*