Itoshe kufungia vyombo vya habari – Meena

Neville Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, sehemu ya sheria ya magazeti ya Mwaka 1976, imetumika kufungia magazeti kwa miaka 40 na kwamba, ‘kazi’ hiyo imepokewa na sheria ya 2016.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Kipindi cha Front Page kinachorushwa na Radio pia Global Televisheni, leo tarehe 13 Septemba 2022, jijini Dar es Salaam.

 

‘‘Sheria ya Habari ya Mwaka 1976, imefanya kazi kwa miaka 40, muda wote huo imetoa mwanya kwa mtu mmoja (waziri) kufungia chombo cha habari anapojisikia kufanya hivyo.

‘‘Hata Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipotungwa, imefuata mkondo huo huo wa kutoa mamlaka kwa mtu mmoja kuamua kufungia chombo cha habari ama la! ingawa mamlaka hayo amepewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo! Katika mabadiliko haya, tumeiomba serikali iondoe kipengele hicho,’’ alisema Meena.

Amesema, katika mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Habari wa sasa, wadau wamelenga kuondoa vikwanzo katika utendaji wa kila siku wa wanahabari.

Amesema, mapendekezo ya wadau wa habari yamegusa vipengele vyote vya sheria na sasa mchakato wa kubadili sheria hiyo unaendelea.

 

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*