Mchakato mabadiliko sheria za habari ulianza mapema – Meena

NEVILLE Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ametembelea vyombo vya habari vya Nyemo FM na Mwangaza FM jijini Dodoma, kuelezea mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Kwenye mazungumzo na vyombo hivyo, Meena amesema, Sheria za Habari za Mwaka 2016 zilianza kupingwa siku moja baada ya kusainiwa na kuanza kutumika.

“Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipitishwa katika mazingira ambayo sisi wadau wa habari hatukuridhika, maeneo mengi ya msingi ambayo tuliyataka yawe sehemu ya sheria hiyo yaliachwa,” amesema Meena na kuongeza;

“Baada ya sheria hizi kupita na wadau kutokubaliana nazo, tulianza kudai mabadiliko lakini katika utawala uliopita hatukuona juhudi zozote zikifanywa na serikali.”

.

Meena akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari katika Kituo cha Radio cha Nyemo (Nyemo FM), jijini Dodoma.

Meena akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari katika Kituo cha Radio cha Mwangaza (Mwangaza FM), jijini Dodoma.

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*