BRELA yatoa somo ‘Umiliki Manufaa’ kwa Wahariri

Kampuni zote zilizosajiliwa Tanzania, baada ya siku 30 lazima ziwasilishe majina ya wanufaa wake ‘Umiliki Manufaa’. Hili ni hitajio la kisheria.

Ni kauli ya Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Meinrad Rweyemamu akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini leo tarehe 8 Juni 2023, jijini Dar es Salaam.

“Kila kampuni inapaswa kuwasilisha majina ya wanufaika wake baada ya siku 30 kusajiliwa, nchi nyingine wanafanya siku hiyo hiyo ya usajili lakini sisi walau tumeweka siku 30 baada ya kusajiliwa.

“Kutofanya hivyo utalazimika kulipa faini. Sheria hii imeanza kutumika baada ya marekebisho ya sheria ya Kampuni Sura 212, mwaka 2022 na ndipo ilipotambulisha dhana ya Mmiliki Manufaa,” amesema.

EditorsForums

Kwenye warsha hiyo, mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ambaye baada ya kufungua warsha hiyo, alisema kanuni zake ‘Umilili Manufaa’ zilianza kutumika mwaka 2022 baada ya sheria hiyo kupitishwa mwaka huo huo.

“Hii ni dhana mpya, BRELA imeanza kukusanya taarifa ingawa kampuni zingine hazijafanya hivyo, tufanye hivyo. Warsha hii inalenga kueleza taratibu na umuhimu wa uwasilishaji taarifa za kampuni kwa BRELA kuhusu umiliki manufaa,” amesema.

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*