Balozi Uholanzi: Uhuru wa habari ni moyo wa demokrasia

UHURU wa vyombo vya habari ni muhimu katika kukuza demokrasia ya kweli. Vyombo vya habari huru ndio msingi wa kuibua mijadala mizito, hutoa muongozo katika utungaji wa sheria na mwelekeo chanya wa taifa.

Ni kauli ya Wiebe Jakob de Boer, Balozi wa Netherland nchini Tanzania wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari zinazohusu mabadiliko ya Sheria ya Habari nchini.

Semina hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ilifanyika katika Hoteli ya Slip Way, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deodatus Balile.

Akifungua mkutano huo, Balozi Boer alisema uhuru wa vyombo vya habari ndio moyo wa demokrasia ya nchi yoyote kwa kuwa, hutoa mwanga na mwelekeo wa taifa.

Balozi huyo alisema, mamlaka zikijenga tabia ya kusikiliza sauti za watu wote na kuchukua mawazo kwa kiwango kikubwa, itasaidia katika kufanya uamuzi wenye manufaa kwa wananchi na taifa.

‘‘Tunaamini kwamba, uwepo wa tabia ya kusikiliza sauti zote na kusikiliza mawazo ya kila mtu, inawezesha kufanya uamuzi wenye busara kwa manufaa ya taifa sambamba na kuinua maisha ya wananchi wote,’’ alisema Balozi Boer.

Kwenye semina hiyo, Balile alimueleza Balozi Boer utayari wa serikali katika safari ya mabadiliko ya sheria ya habari.

Alieleza mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari unahusisha taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jamii Forums.

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*