AG Feleshi: Tupo pamoja mabadiliko ya sheria ya habari

JAJI Eliezer Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), amesema yupo pamoja na wanahabari katika safari ya mabadiliko ya sheria zinazohusu tasnia ya habari nchini.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Juni 2022, ofisini kwake bungeni, jijini Dodoma alipokutana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na wadau wengine wa habari.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Amesema, katika mabadiliko ya haraka, kuna mambo mengi yaliyotokea na makovu yake hayawezi kufutika kwa haraka.

“Sishangai yote yaliyotokea hapa katikati katika kipindi cha transformation (mabadiliko), katika mabadiliko ya haraka, makovu huwa hayafutiki haraka,” amesema Jaji Feleshi.

Amesema, ingawa serikali hujilinda lakini sheria zinapaswa kuwa na uhalali na malengo kwa wananchi.
“Kila serikali huwa inajilinda, hakuna serikali isiyojilinda,” amesema Jaji Feleshi.
Jaji huyo amesema, sheria yoyoye inayoundwa nchini, lazima iwe na uhalali, malengo ya nchi na wananchi pia.
Jaji Feleshi ametoa kauli hiyo baada ya Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF kumweleza baadhi ya sheria za habari zilizotengenezwa namna zinavyominya uhuru wa habari na wanahabari nchini.

Miongoni mwa kasoro hizo ni pamoja na mwanahabari kuweza kufungwa bila hata kuitwa mahakanai kujitetea, kuundwa vyombo vingi vitakavyoelemea wanahabari, dhana kutumika kufunga wanahabari lakini pia vyombo vya habari kufungwa bila kufikishwa mahakamani.

Jaji Feleshi amesema, ni vizuri kwa tasnia ya habari kuwa na bodi yake itakayotumika kuhakikisha inasimamia maadili ya wanahabari.
“Sina tatizo, naona muwe na ‘regulator’, bodi yenu moja, ili mmoja wenu akienda kinyume na maadili (ya uandishi wa habari), mnamshughulikia nyinyi wenyewe,” amesema Jaji Eliezer Feleshi.
“Niko na nyinyi na Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) katika hatua kuelekea mabadiliko ya sheria za habari.

James Marenga, Makamu Mwenyekiti wa MISA- TAN, amemweleza Jaji Feleshi kuwa, wadau wa habari wanashirikiana ili kufika malengo ya mabadiliko ya sheria zinazominya uhuru wa habari nchini.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tangaza nasi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*